IQNA

Njama za Adui

Kamanda wa IRGC: Stratejia hatari ya adui ni hujuma dhidi ya akili

8:14 - August 22, 2022
Habari ID: 3475661
TEHRAN (IQNA)- Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) ametahadharisha kuwa, stratejia hatari zaidi ambayo adui ameamua kutumia ni vita vya kinafsi na kisaikolojia.

Brigedia Jenerali Hossein Salami alisema hayo jana Jumapili hapa Tehran na kueleza kuwa, "Hii leo, lugha (maneno) na kalamu (maandishi) ndio silaha inayoweza kutotoa kwa mafanikio katika nafsi ya vita vikubwa. Adui ametumia njia zote ili kutufanya tusalimu amri, na kuanzisha vita vya kila namna bila mafanikio." 

Amesema maadui wametumia nguvu zao za kijeshi kadri wanavyoweza, sambamba na kutumia mashinikizo ya kiuchumi na silaha zote za maangamivu kujaribu kuzima irada ya taifa la Iran, lakini hawajafanikiwa.

Jenerali Salami amebainisha kuwa, kitendo cha maadui kuanzisha vita vya kiintelijensia dhidi ya Iran, mauaji ya kigaidi na hujuma dhidi ya mfumo wa usalama wa ndani wa nchi hii, yote hayo yamegonga mwamba.

Kamanda Mkuu wa Jeshi la IRGC la Iran amesisitiza kuwa, hujuma ya maadui dhidi ya nafsi na akili, ndio stratejia ya hatari zaidi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Ameongeza kwa kusema: Walimu wetu ni wacha-Mungu, wenye hulka na tabia njema, wana akhlaqi na mienendo safi ya kuweza kuvijenga vizazi vya vijana katika misingi ya sayansi na nadharia ya elimu.

4079648

captcha