IQNA

Mbinu ya Elimu ya Manabii; Nuh/37

Kutafakari Katika Mbinu ya Elimu ya Nabii Nuh

16:08 - November 30, 2023
Habari ID: 3477966
TEHRAN (IQNA) – Ujinga na kukataa kufikiri na kutafakari ni uhalifu ambao umesababisha madhara kwa ubinadamu katika historia.

Ikiwa hazitazuiwa, hata njia bora za elimu zinazotumiwa na walimu bora na waelimishaji hazitakuwa na matunda.

Kama vile tulivyotambua kuwepo kwa uelewa kwa wanadamu, tunapaswa kuzingatia njia ya kuelewa kwao pia. Hapa kuna mifano miwili ya njia kama hizo:

  • Mwanadamu anaweza kutambua mambo na kutofautisha sahihi na isiyo sahihi na nzuri kutoka mbaya kwa kutumia hisia zake tano. Kwa hivyo hisia ni njia ya kuelewa.
  • Akili na mantiki. Akili ni chombo cha utambuzi ambacho kina uwezekano mdogo kuliko hisi kufanya makosa. Walakini, akili pia hukumbwa na makaosa katika maamuzi.

Akili na mantiki hutumika sana katika elimu. Ufahamu, ambao ni mojawapo ya vipengele muhimu vya elimu, hupitishwa kutoka kwa mwalimu hadi kwa yule anayepokea elimu kupitia akili.

Nabii Nuh (AS) alitumia njia ya hoja na kutafakari kuwaelimisha watu wake na kuwaongoza kwenye njia iliyonyooka.

Aliwatajia sababu mbalimbali za kuumbwa kwa mbingu na dunia na kuumbwa kwa wanadamu, ili kuwathibitishia kwamba kuna uhitaji wa kuwa na Muumba. Wao, hata hivyo, walikataa sababu na hoja hizo imara.

Hapa kuna mifano miwili ya mfumo wa kutafakari wa Nabii Nuh:

  • Uumbaji wa mwanadamu

Nuh (AS) kwa mara ya kwanza alirejelea uumbaji wa wanadamu: “Mna nini hamweki heshima ya Mwenyezi Mungu?  Na hali Yeye kakuumbeni daraja baada ya daraja?” (Aya 13-14 za Surah Nuh)

Anarejelea hatua za uumbaji ili kuonyesha jinsi Mwenyezi Mungu amewaumba wanadamu.

Kwa mujibu wa Aya ya 14 ya Surah Muminoun, hizi ni hatua za kuumbwa kwa mwanadamu: “Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama. Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa waumbaji. "

  • Uumbaji wa mbingu

Hoja nyingine iliyotumiwa na Nuhu (AS) ni ile inayohusiana na uumbaji wa mbingu saba:

"  Kwani hamwoni jinsi Mwenyezi Mungu alivyo ziumba mbingu saba kwa matabaka?" (Aya ya 15 ya Surah Nuh)

Ni dhahiri kwamba ikiwa watu wote watakusanyika pamoja, hawataweza kuumba mbingu ya kwanza ambayo inaonekana kwetu, na mbingu nyingine. Kwa hiyo sanamu, ambazo zimetengenezwa na mwanadamu, zinawezaje kuwa muumbaji wa mbingu?

Habari zinazohusiana
Kishikizo: nuhu
captcha