IQNA

Jiografia ya Matukio katika Qur'ani Tukufu /2

Watu wa Nabii Nuhu waliishi wapi?

7:20 - December 12, 2023
Habari ID: 3478025
IQNA – Kisha cha Nabii Nuh au Nuhu (AS) ni miongoni mwa visa muhimu vilivyotajwa ndani ya Qur'ani Tukufu na kuna sura maalum, Surah Nuh, iliyowekwa kwa ajili ya Mtume huyu wa Mwenyezi Mungu na watu wake.

Kwa kuzingatia maisha yake marefu, yaliyodumu takriban miaka 1,000, Nabii Nuhu (AS) alishuhudia matukio mengi wakati wa utume wake yaliyotokea katika maeneo tofauti ya kijiografia.

Mwenyezi Mungu anasema katika Aya ya 1-4 ya Sura Nuh: “ Hakika Sisi tulimtuma Nuh'u kwa watu wake: Uwaonye kaumu yako kabla ya kuwafikia adhabu chungu. Akasema: Enyi watu wangu! Kwa hakika mimi ni mwonyaji wa dhaahiri kwenu. Ya kwamba mumuabudu Mwenyezi Mungu, na mumche Yeye, na mumt'ii. Atakughufirieni madhambi yenu, na atakuakhirisheni mpaka muda ulio wekwa. Hakika muda wa Mwenyezi Mungu utapo fika haucheleweshwi. Laiti mngejua!’”

Nuhu (AS) aliteuliwa kuwa utume baada ya Shayth (AS) na Idris (AS). Alikuwa Mtume Ul-ul-Adhm (Waliotukuzwa zaidi kuliko wengine) na ndiye aliyeishi muda mrefu zaidi. Nuh (AS) alikuwa seremala.

Aliwaalika watu wake kumwabudu Mungu mmoja na akawaonya dhidi ya kuabudu masanamu. Matajiri waliokuwa na inda na kiburi walimtuhumu kuwa amepotea.

“Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku iliyo kuu. Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika upotofu ulio dhaahiri. Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.” (Aya 59 -61 ya Surat Al-A'araf)

Baada ya watu kukataa kuamini hata baada ya miaka mingi ya kueneza ukweli, Nuhu (AS) alipewa jukumu la kujenga safina au chombo cha kuwaokoa waumini na wanyama kutokana na mafuriko yanayokuja.

Sasa swali ni mahali alipoishi Nuhu (AS) na watu wake. Je! alijenga wapi Safina yake?

Imesemekana kwamba Msikiti wa Kufa (katika Iraq ya leo) ulikuwa ni mahali ambapo Nuhu (AS) alimuabudu Mwenyezi Mungu na kuswali.

Pia inasemekana alijenga Safina yake katika mji huo wa Kufa, ulioko kilomita 12 kaskazini mwa Najaf, kusini mwa Iraq.

Waislamu wanaamini kwamba Msikiti wa Kufa ulijengwa kwa mara ya kwanza na Mtume Adam (AS).

Msikiti wa Kufa ni miongoni mwa misikiti minne kuu katika ulimwengu wa Kiislamu. Fadhila nyingi zimehusishwa na msikiti huu. Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (AS) amesema: Majumba manne kutoka katika kasri za peponi yapo hapa duniani na ni Msikiti Mkuu wa Makka, Msikiti wa Mtume katika mji wa Madina, Msikiti wa Al-Aqsa huko al-Quds na Msikiti wa Kufa.

Kishikizo: nuhu Kufa
captcha